Friday, 19 September 2014

Uzuri wa Katavi

Katavi ni moja ya hifadhi ya Taifa iliyopo Wilayani Mpanda, Mkoani Katavi. Hifadhi hii inasadikiwa kuwa ya tatu kwa ukubwa wake kati ya hifadhi zilizopo hapa  Nchini Tanzania

Pamoja na Mbuga ya Katavi kubeba Wanyama wengi ndani yake bado kuna vyanzo mbalimbali ambapo vinazidi kupendezesha Mbuga hiyo, ambapo Mito midogo midogo ndani yake nayo inatiririsha maji yake katika Ziwa Rukwa
Hifadhi ya Mbuga ya Katavi ikionekana na wanyama wapatikanao pamoja na Mito iliyopo ndani yake.
Watalii wengi wanafika Nchini kuangalia uzuri wa Hifadhi ya Katavi. Je? Watanzania wangapi wana desturi ya kutembelea hifadi zilizopo Nchini. Wanyama kama Twiga ni kati ya Wanyama wanaopatikana ndani ya Katavi na kwa uzuri wa Twiga ni kweli Katavi inastahili kupendeza na kuitwa Mbuga yenye kuvutia

Twiga Mnyama mwenye kuvutia ndani ya Hifadhi ya Katavi.
Tembo wapatikanao ndani ya hiadhi ya Katavi  wakinywa maji katika Mto upatikanao ndani ya Katavi.