Tanzania ni miongoni mwa Nchi zilizobahatika kuwa na hifadhi zenye wanyama wazuri na wanaopendwa sana duniani. miongoni mwa wanyama hao ni Tembo na Twiga ambao wanapatikana karibu ndani ya hifadhi zote za hapa nchini.
Miaka ya hivi karibuni kumeibuka majangili ambao wanafanya biashara haramu ya kuua Wanyama hao na kuwasafirisha nje ya nchi , wakati mwingine kuwaua na kuchukua sehemu za miili yao kama pembe na meno yao ambayo yameonekana kuwa na thamani kubwa sana.
Pamoja na hayo wanaharakati pamoja viongozi wa Nchi wameonesha uzalendo kwa kupiga vita mauaji hayo ambayo kwa ujumla yanachafua sifa ya Tanzania na hata wakati mwingine kunapelekea watalii kukata tamaa ya kufika nchini kwani ule uzuri wa mbuga wa kuvutia umekua unapotea kwa wanyama Tembo na Twiga ambao ndio wanawindwa kutoonekana kwa wingi.
Tembo ni wanyama wenye Thamani sana kwani meno yake mawili ni kama lulu kwa majangili ambao kila kukicha wanazidi kuwawinda na bila huruma kutumia silaha kama bunduki kwa ajili ya kuwawinda hali inayopelekea kuishi kwa wasi wasi mkubwa wawapo hifadhini
Swali linakuja kuwa je? ni kina nani wanahsika na Ujangili huu hatari sana, Mbuga zote zina walinzi ambao wameaminiwa na Serikali kwa ajili ya kulinda Nyara hizo Je majangili hao wanapenyaje na kuondoka na Wanyama hao bila majangili kujulikana nawalinzi kutodhurika? haya yanawezekana ni maswali ambayo kila mwananchi anajiuliza na majibu yake bado ni kitendawili kwa Taifa zima.
Ni jukumu la kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake na hata wakati mwingine kutoa taarifa iwapo unahisi kuna tendo au mtu mwenye matendo ya kijangili ili kuweza kuwanusuru wanyama hawa wachache waliobaki hapa nchini kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Takwimu mbalimbali zinathibitisha kwamba ndani ya mwaka mmoja zaidi ya
Tembo 500 wanauawa hali inayopelekea hifadhi kubwa kama ya Ruaha na
Serengeti kubaki na tembo wachache sana kuliko hapo awali hali
inayotishia miaka ijayo wanyama hao wanaweza kupotea kabisa katika
hifadhi hapa nchini. Bofya hapa kwa ufafanuzi zaidi http://archive.habarileo.co.tz/index.php/makala/20883-tanzania-bila-tembo-haiwezekani
Wednesday, 22 October 2014
Friday, 3 October 2014
warembo na utalii
miss utalii
Mashindano ya kumsaka miss utalii 2014/2015 yanarudi tena baada ya kusimama kwa mwaka mmoja kutokana na mipango ya awali kuwa na udhaifu katika kufanya maamuzi na kutafuta warembo wenye vigezo vya kuiwakilisha vyema TanzaniaMashindano ya Urembo Tanzania ni mashindano yenye kubeba vigezo mbali mbali vya warembo hapa nchini. Ndani ya mashindano hayo yamegawanyika katika makundi tofauti tofauti na yote yakiwa yana lengo kubwa moja la kumtoa mrembo awakalishe Nchi vyema kimataifa
Miss utalii ni shindano linalomhusu mrembo wa kuuwakilisha utalii wa ndani ya nchini kimataifa kama jina la shindano lilivyo.Mara nyingi shindano hilo litahusisha warembo kutembelea hifadhi mbalimbali zilizopo ndani ya nchi
Mashindano haya hayafiki mbali kutokana na kwamba warembo hawapatiwi mafunzo ya kutosha juu ya shindano linahusu nini hivyo kushindwa kuiwakilisha nchi kama jinsi inavyotakiwa kufanyika kimataifa na pia kutokupewa mafunzo na hata baada ya shindano kumalizika.
warembo waliofanikiwa kuingia tano bora Miss utalii 2012/2013 katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Tanga Bi.Halima Bendego |
Hata hivyo warembo wa mashindano haya bado hawajapewa nafasi au thamani kama inayowapasa kutokana na kuwakilisha Nchi kwa utambulisho wa utalii wa ndani na badala yake kubaki kuendelea kutaabika pamoja na kuwa na taji kubwa la kama mrembo wa Utalii Tanzania
Khadija Saidi akivalishwa taji la Miss Utalii Tanzania 2012/2013 na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Tanga Bi.Halima Bendego kabla ya mashindano hayo kufungwa kwa mwaka mmoja |
Miss utalii tatu bora 2012/2013.katikati ni mshindi wa kwanza Khadija Said kulia ni Lucy Noel mshindi wa pili na kushoto ni Thelecia Kilomoa mshindi wa tatu |
Friday, 19 September 2014
Uzuri wa Katavi
Katavi ni moja ya hifadhi ya Taifa iliyopo Wilayani Mpanda, Mkoani Katavi. Hifadhi hii inasadikiwa kuwa ya tatu kwa ukubwa wake kati ya hifadhi zilizopo hapa Nchini Tanzania
Pamoja na Mbuga ya Katavi kubeba Wanyama wengi ndani yake bado kuna vyanzo mbalimbali ambapo vinazidi kupendezesha Mbuga hiyo, ambapo Mito midogo midogo ndani yake nayo inatiririsha maji yake katika Ziwa Rukwa![]() | |
Hifadhi ya Mbuga ya Katavi ikionekana na wanyama wapatikanao pamoja na Mito iliyopo ndani yake | . |
![]() |
Twiga Mnyama mwenye kuvutia ndani ya Hifadhi ya Katavi. |
![]() |
Tembo wapatikanao ndani ya hiadhi ya Katavi wakinywa maji katika Mto upatikanao ndani ya Katavi. |
Subscribe to:
Posts (Atom)