Tanzania ni miongoni mwa Nchi zilizobahatika kuwa na hifadhi zenye wanyama wazuri na wanaopendwa sana duniani. miongoni mwa wanyama hao ni Tembo na Twiga ambao wanapatikana karibu ndani ya hifadhi zote za hapa nchini.
Miaka ya hivi karibuni kumeibuka majangili ambao wanafanya biashara haramu ya kuua Wanyama hao na kuwasafirisha nje ya nchi , wakati mwingine kuwaua na kuchukua sehemu za miili yao kama pembe na meno yao ambayo yameonekana kuwa na thamani kubwa sana.
Pamoja na hayo wanaharakati pamoja viongozi wa Nchi wameonesha uzalendo kwa kupiga vita mauaji hayo ambayo kwa ujumla yanachafua sifa ya Tanzania na hata wakati mwingine kunapelekea watalii kukata tamaa ya kufika nchini kwani ule uzuri wa mbuga wa kuvutia umekua unapotea kwa wanyama Tembo na Twiga ambao ndio wanawindwa kutoonekana kwa wingi.
Tembo ni wanyama wenye Thamani sana kwani meno yake mawili ni kama lulu kwa majangili ambao kila kukicha wanazidi kuwawinda na bila huruma kutumia silaha kama bunduki kwa ajili ya kuwawinda hali inayopelekea kuishi kwa wasi wasi mkubwa wawapo hifadhini
Swali linakuja kuwa je? ni kina nani wanahsika na Ujangili huu hatari sana, Mbuga zote zina walinzi ambao wameaminiwa na Serikali kwa ajili ya kulinda Nyara hizo Je majangili hao wanapenyaje na kuondoka na Wanyama hao bila majangili kujulikana nawalinzi kutodhurika? haya yanawezekana ni maswali ambayo kila mwananchi anajiuliza na majibu yake bado ni kitendawili kwa Taifa zima.
Ni jukumu la kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake na hata wakati mwingine kutoa taarifa iwapo unahisi kuna tendo au mtu mwenye matendo ya kijangili ili kuweza kuwanusuru wanyama hawa wachache waliobaki hapa nchini kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Takwimu mbalimbali zinathibitisha kwamba ndani ya mwaka mmoja zaidi ya
Tembo 500 wanauawa hali inayopelekea hifadhi kubwa kama ya Ruaha na
Serengeti kubaki na tembo wachache sana kuliko hapo awali hali
inayotishia miaka ijayo wanyama hao wanaweza kupotea kabisa katika
hifadhi hapa nchini. Bofya hapa kwa ufafanuzi zaidi http://archive.habarileo.co.tz/index.php/makala/20883-tanzania-bila-tembo-haiwezekani
No comments:
Post a Comment