miss utalii
Mashindano ya kumsaka miss utalii 2014/2015 yanarudi tena baada ya kusimama kwa mwaka mmoja kutokana na mipango ya awali kuwa na udhaifu katika kufanya maamuzi na kutafuta warembo wenye vigezo vya kuiwakilisha vyema TanzaniaMashindano ya Urembo Tanzania ni mashindano yenye kubeba vigezo mbali mbali vya warembo hapa nchini. Ndani ya mashindano hayo yamegawanyika katika makundi tofauti tofauti na yote yakiwa yana lengo kubwa moja la kumtoa mrembo awakalishe Nchi vyema kimataifa
Miss utalii ni shindano linalomhusu mrembo wa kuuwakilisha utalii wa ndani ya nchini kimataifa kama jina la shindano lilivyo.Mara nyingi shindano hilo litahusisha warembo kutembelea hifadhi mbalimbali zilizopo ndani ya nchi
Mashindano haya hayafiki mbali kutokana na kwamba warembo hawapatiwi mafunzo ya kutosha juu ya shindano linahusu nini hivyo kushindwa kuiwakilisha nchi kama jinsi inavyotakiwa kufanyika kimataifa na pia kutokupewa mafunzo na hata baada ya shindano kumalizika.
warembo waliofanikiwa kuingia tano bora Miss utalii 2012/2013 katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Tanga Bi.Halima Bendego |
Hata hivyo warembo wa mashindano haya bado hawajapewa nafasi au thamani kama inayowapasa kutokana na kuwakilisha Nchi kwa utambulisho wa utalii wa ndani na badala yake kubaki kuendelea kutaabika pamoja na kuwa na taji kubwa la kama mrembo wa Utalii Tanzania
Khadija Saidi akivalishwa taji la Miss Utalii Tanzania 2012/2013 na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Tanga Bi.Halima Bendego kabla ya mashindano hayo kufungwa kwa mwaka mmoja |
Miss utalii tatu bora 2012/2013.katikati ni mshindi wa kwanza Khadija Said kulia ni Lucy Noel mshindi wa pili na kushoto ni Thelecia Kilomoa mshindi wa tatu |
No comments:
Post a Comment